Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 4:24 - Swahili Revised Union Version

24 watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, na ili nanyi mpate kumcha BWANA, Mungu wenu, milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 ili watu wote wa dunia wajue kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu una nguvu; nanyi mpate kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 ili watu wote wa dunia wajue kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu una nguvu; nanyi mpate kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 ili watu wote wa dunia wajue kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu una nguvu; nanyi mpate kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, milele.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Alifanya hivi ili mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa Mwenyezi Mungu ni wenye nguvu, na ili kila wakati mpate kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa bwana ni wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumcha bwana Mwenyezi Mungu wenu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

24 watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, na ili nanyi mpate kumcha BWANA, Mungu wenu, milele.

Tazama sura Nakili




Yoshua 4:24
24 Marejeleo ya Msalaba  

ili wakuche wewe siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.


Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa BWANA ndiye Mungu; hakuna mwingine.


Basi sasa, Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA Mungu, wewe peke yako.


Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani kote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee zawadi kutoka mtumwa wako.


Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.


Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?


Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, Ayadhihirishe matendo yake makuu.


Mkono wako ni mkono wenye uweza, Mkono wako una nguvu, Mkono wako wa kulia umetukuka.


Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.


Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.


Hofu na woga zimewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.


Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.


lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuoneshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.


BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.


nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu mioyoni mwao, ili wasiniache.


Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.


upate kumcha BWANA, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe.


Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo