Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
Yoshua 19:49 - Swahili Revised Union Version Basi walipomaliza kazi yao hiyo ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kufuata mipaka yake; wana wa Israeli kakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao. Biblia Habari Njema - BHND Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao. Neno: Bibilia Takatifu Walipomaliza kuigawa nchi kulingana na sehemu zilizowaangukia, Waisraeli walimpa Yoshua mwana wa Nuni urithi kati yao, Neno: Maandiko Matakatifu Walipomaliza kugawanya nchi katika migawo kulingana na sehemu zao zilizowaangukia, Waisraeli wakampa Yoshua mwana wa Nuni urithi katikati yao, BIBLIA KISWAHILI Basi walipomaliza kazi yao hiyo ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kufuata mipaka yake; wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao; |
Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.
kulingana na ile amri ya BWANA wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo.
Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.