Basi sasa hiyo ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, aliyonena bwana wangu, na wapelekewe watumishi wake;
Yoshua 19:46 - Swahili Revised Union Version Meyarkoni na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Me-yarkoni na Rakoni na nchi iliyokuwa karibu na Yopa. Biblia Habari Njema - BHND Me-yarkoni na Rakoni na nchi iliyokuwa karibu na Yopa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Me-yarkoni na Rakoni na nchi iliyokuwa karibu na Yopa. Neno: Bibilia Takatifu Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa. Neno: Maandiko Matakatifu Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa. BIBLIA KISWAHILI Meyarkoni na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa. |
Basi sasa hiyo ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, aliyonena bwana wangu, na wapelekewe watumishi wake;
nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaipeleka Yerusalemu.
Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akateremka hadi Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akalipa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.
Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.
Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi waliosikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Njoo kwetu pasipo kukawia.
Basi Petro akakaa siku kadhaa huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.
Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao.