Yoshua 19:35 - Swahili Revised Union Version Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Miji yao iliyokuwa na ngome ni Zidimu, Zeri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, Biblia Habari Njema - BHND Miji yao iliyokuwa na ngome ni Zidimu, Zeri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Miji yao iliyokuwa na ngome ni Zidimu, Zeri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, Neno: Bibilia Takatifu Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, Neno: Maandiko Matakatifu Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, BIBLIA KISWAHILI Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi; |
Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za BWANA, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne.
Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
Basi wakapanda wakaipeleleza nchi toka jangwa la Sini hadi Rehobu, mpaka kuingia Hamathi.
na kutoka mlima wa Hori mtaweka alama hadi Hamathi; na kutokea kwake mpaka hadi hapo Sedada;
na nchi ya Araba nayo, na mto wa Yordani, na mpaka wake, tokea Kinerethi mpaka bahari ya hiyo Araba, nayo ni Bahari ya Chumvi, chini ya materemko ya Pisga, upande wa mashariki.
na hao wafalme waliokuwa upande wa kaskazini, katika nchi ya vilima, na katika Araba upande wa kusini wa Kinerethi, na katika Shefela, na katika nchi tambarare za Dori upande wa magharibi,
tena katika bonde, Beth-haramu, na Bethnimira, na Sukothi, na Safoni, hiyo iliyosalia ya ufalme wa Sihoni mfalme wa Heshboni, yaani mto wa Yordani na kingo zake, mpaka mwisho wa bahari ya Kinerethi ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki.
tena mpaka ulizunguka kwendelea upande wa magharibi hadi Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikia hadi Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikia hadi Asheri upande wa magharibi, tena ulifikia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea maawio ya jua.
Nao wakaweka Kedeshi katika Galilaya katika nchi ya vilima ya Naftali, na Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-arba (ndio Hebroni) katika nchi ya vilima ya Yuda.
Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu.
Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.