Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Yoshua 19:10 - Swahili Revised Union Version Kisha sehemu ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikia hadi Saridi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kura ya tatu ilizipata koo za kabila la Zebuluni. Eneo lao lilienea hadi Saridi. Biblia Habari Njema - BHND Kura ya tatu ilizipata koo za kabila la Zebuluni. Eneo lao lilienea hadi Saridi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kura ya tatu ilizipata koo za kabila la Zebuluni. Eneo lao lilienea hadi Saridi. Neno: Bibilia Takatifu Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, kufuatana na koo zao: Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. Neno: Maandiko Matakatifu Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. BIBLIA KISWAHILI Kisha sehemu ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikia hadi Saridi; |
Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
Na mpakani mwa Isakari, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Zabuloni, fungu moja.
Kisha ilizuka kura ya kabila la wana wa Benyamini kwa kulingana na jamaa zao; na mpaka wa hiyo kura yao ukatokea kati ya wana wa Yuda na wana wa Yusufu.
Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia kura hapa mbele ya BWANA, Mungu wetu.
kisha mpaka wao ukakwea kwendelea upande wa magharibi, hadi kufikia Marala, nao ukafikia hadi Dabeshethi; nao ukafikia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu;
Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.