na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi;
Yoshua 15:41 - Swahili Revised Union Version Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema - BHND Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Neno: Bibilia Takatifu Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake. Neno: Maandiko Matakatifu Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake. BIBLIA KISWAHILI Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. |
na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi;
Wafilisti pia walikuwa wameishambulia na kuitwaa miji ya Shemeshi, Ayaloni, Gederothi, soko, pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake na Gimzo pia na vijiji vyake, miji yake; wakakaa humo.
Basi ikawa hao marafiki watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumfariji Ayubu na kumtuliza moyo.
BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hadi kufikia Azeka, tena hadi kufikia Makeda.
ndipo hao watu wote wakamrudia Yoshua kambini huko Makeda salama; hakuna mtu awaye yote aliyetoa ulimi kinyume cha hao wana wa Israeli hata mmojawapo.
Siku hiyo Yoshua akautwaa mji wa Makeda, akaupiga kwa makali ya upanga, na mfalme wake; akawaangamiza kabisa na wote pia waliokuwamo ndani yake, hakumwacha hata mmoja aliyesalia; naye akamfanyia huyo mfalme wa Makeda kama alivyomfanyia huyo mfalme wa Yeriko.
kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikia hadi Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hadi Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hadi Kabuli upande wa kushoto;