Akamwambia, Nenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akamtuma kutoka bonde la Hebroni, na akafika Shekemu.
Yoshua 14:14 - Swahili Revised Union Version Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi hata hivi leo, kwa sababu, alikuwa mwaminifu kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, mji wa Hebroni ni sehemu yao wazawa wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi mpaka hivi leo, kwa sababu Kalebu alikuwa mwaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, mji wa Hebroni ni sehemu yao wazawa wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi mpaka hivi leo, kwa sababu Kalebu alikuwa mwaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, mji wa Hebroni ni sehemu yao wazawa wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi mpaka hivi leo, kwa sababu Kalebu alikuwa mwaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Hebroni imekuwa mali ya Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandama Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Hebroni imekuwa mali ya Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandama bwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi hata hivi leo, kwa sababu, alikuwa mwaminifu kwa BWANA, Mungu wa Israeli. |
Akamwambia, Nenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akamtuma kutoka bonde la Hebroni, na akafika Shekemu.
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa makabila yao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.
Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriath-arba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao Waanaki. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.