Yoshua 13:2 - Swahili Revised Union Version Nchi iliyosalia ni hii; nchi zote za Wafilisti, na Wageshuri wote; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sehemu hizo ni: Nchi yote ya Wafilisti na nchi yote ya Wageshuri, Biblia Habari Njema - BHND Sehemu hizo ni: Nchi yote ya Wafilisti na nchi yote ya Wageshuri, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sehemu hizo ni: nchi yote ya Wafilisti na nchi yote ya Wageshuri, Neno: Bibilia Takatifu “Nchi iliyosalia ni hii: “maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: Neno: Maandiko Matakatifu “Nchi iliyosalia ni hii: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: BIBLIA KISWAHILI Nchi iliyosalia ni hii; nchi zote za Wafilisti, na Wageshuri wote; |
Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Abrahamu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.
Maana mimi mtumishi wako niliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama BWANA akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia BWANA.
na wa pili wake Danieli, wa Abigaili mkewe Nabali wa Karmeli; na wa tatu Absalomu, mwana wa Maaka binti Talmai, mfalme wa Geshuri,
Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lolote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la BWANA liko juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako.
Yairi, mwana wa Manase, alitwaa nchi yote ya Argobu, hata mpaka wa Wageshuri na Wamaaka; akaziita nchi hizo Hawoth-yairi, kwa jina lake mwenyewe, hata hivi leo, maana, hizo nchi za Bashani.)
naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hadi mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni.
na Gileadi na mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na mlima wa Hermoni wote, na Bashani yote mpaka Saleka;
Pamoja na hayo wana wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri, wala Wamaaka; lakini Wageshuri na Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hadi siku hii ya leo.
Basi haya ndiyo mataifa ambao BWANA aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani, awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani;
Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, mpaka nchi ya Misri.