Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Sefania 2:5 - Swahili Revised Union Version

5 Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la BWANA liko juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Ole wenu wakazi wa nchi za pwani, watu mnaoishi huko Krete! Mwenyezi-Mungu ametamka dhidi yenu enyi wakazi wa Kanaani, nchi ya Filistia: Mimi nitawaangamiza asibaki hata mkazi mmoja!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Ole wenu wakazi wa nchi za pwani, watu mnaoishi huko Krete! Mwenyezi-Mungu ametamka dhidi yenu enyi wakazi wa Kanaani, nchi ya Filistia: Mimi nitawaangamiza asibaki hata mkazi mmoja!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Ole wenu wakazi wa nchi za pwani, watu mnaoishi huko Krete! Mwenyezi-Mungu ametamka dhidi yenu enyi wakazi wa Kanaani, nchi ya Filistia: Mimi nitawaangamiza asibaki hata mkazi mmoja!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari, enyi Wakerethi; neno la Mwenyezi Mungu liko dhidi yenu, ee Kanaani, nchi ya Wafilisti. “Mimi nitawaangamiza, na hakuna atakayebaki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari, enyi Wakerethi; neno la bwana liko dhidi yenu, ee Kanaani, nchi ya Wafilisti. “Mimi nitawaangamiza, na hakuna atakayebaki.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la BWANA liko juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako.

Tazama sura Nakili




Sefania 2:5
14 Marejeleo ya Msalaba  

Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7


Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.


Utawezaje kutulia, Ikiwa BWANA amekupa agizo? Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani, Ndipo alipoyaamuru hayo.


kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani.


Lisikieni neno hili alilolisema BWANA juu yenu, enyi wana wa Israeli, juu ya jamaa yote niliowapandisha kutoka nchi ya Misri, nikisema,


Lisikieni neno hili nilitamkalo liwe maombolezo juu yenu, enyi nyumba ya Israeli.


Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote wapimao fedha wamekatiliwa mbali.


Nimekatilia mbali mataifa, minara yao ina ukiwa; nimeziharibu njia kuu zao, hata hapana mmoja apitaye; miji yao imeangamizwa; hamna mtu hata mmoja, wala hapana akaaye huko.


Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.


Nao wakataka kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao.


Nchi iliyosalia ni hii; nchi zote za Wafilisti, na Wageshuri wote;


kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,


aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.


Sisi tulishambulia Negebu ya Wakerethi, na ya milki ya Yuda, na Negebu ya Kalebu; na huo mji wa Siklagi tukauchoma moto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo