Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza.
Yoshua 12:18 - Swahili Revised Union Version mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema mfalme wa Afeka, mfalme wa Lasharoni, Biblia Habari Njema - BHND mfalme wa Afeka, mfalme wa Lasharoni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza mfalme wa Afeka, mfalme wa Lasharoni, Neno: Bibilia Takatifu mfalme wa Afeki; mfalme wa Lasharoni; BIBLIA KISWAHILI mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja; |
Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza.
Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani.
upande wa kusini; nchi yote ya Wakanaani na Meara iliyo ya Wasidoni, mpaka Afeka, hata mpaka wa Waamori;
Basi hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki; nao Waisraeli wakafanya kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli.
[Ikawa siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na Israeli,] nao Waisraeli wakatoka juu ya Wafilisti kwenda vitani; wakatua karibu na Ebenezeri, nao Wafilisti wakatua huko Afeki.