Yoshua 10:42 - Swahili Revised Union Version Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akatwaa kwa wakati mmoja, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliweza kuitwaa nchi hii yote kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, aliwapigania Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Aliweza kuitwaa nchi hii yote kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, aliwapigania Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliweza kuitwaa nchi hii yote kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, aliwapigania Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu Wafalme hawa wote pamoja na nchi zao Yoshua aliwashinda kwa wakati mmoja, kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliwapigania Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Wafalme hawa wote pamoja na nchi zao Yoshua aliwashinda kwa wakati mmoja, kwa sababu bwana, Mungu wa Israeli, aliwapigania Israeli. BIBLIA KISWAHILI Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akawatwaa kwa wakati mmoja, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli, |
Akayakwamisha magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa shida; na Wamisri wakasema, Na tuwakimbieni Waisraeli; kwa kuwa BWANA anawapigania.
Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na makabila ya watu kwa ajili ya maisha yako.
kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizofuata baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.