Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 118:6 - Swahili Revised Union Version

6 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Mwenyezi Mungu yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

Tazama sura Nakili




Zaburi 118:6
20 Marejeleo ya Msalaba  

Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa.


Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,


Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.


Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.


Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.


Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?


Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.


Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?


Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.


Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;


Ni nani atakayesimama Kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayenisaidia Juu yao wafanyao maovu?


Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani?


Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.


Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?


Hata tunathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?


Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana.


Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Nenda, na BWANA atakuwa pamoja nawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo