Yona 4:4 - Swahili Revised Union Version Naye BWANA akasema, Je! Unatenda vema kukasirika? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Mwenyezi-Mungu akamjibu Yona: “Unadhani wafanya vema kukasirika?” Biblia Habari Njema - BHND Naye Mwenyezi-Mungu akamjibu Yona: “Unadhani wafanya vema kukasirika?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Mwenyezi-Mungu akamjibu Yona: “Unadhani wafanya vema kukasirika?” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Mwenyezi Mungu akamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini bwana akamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?” BIBLIA KISWAHILI Naye BWANA akasema, Je! Unatenda vema kukasirika? |
Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula.
Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha; Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze.
Basi, sasa, Ee BWANA, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajitengenezea kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hadi aone mji ule utakuwaje.
Mungu akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa.
Enyi watu wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa kitu gani? Shuhudieni juu yangu.
Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.
Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?