Yeye akaurudisha mpaka wa Israeli toka kuingia kwa Hamathi hata bahari ya Araba, sawasawa na neno la BWANA, Mungu wa Israeli, alilolinena kwa mkono wa mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii, aliyekuwa wa Gath-heferi.
Yona 1:1 - Swahili Revised Union Version Basi neno la BWANA lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku moja, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yona, mwana wa Amitai: Biblia Habari Njema - BHND Siku moja, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yona, mwana wa Amitai: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku moja, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yona, mwana wa Amitai: Neno: Bibilia Takatifu Neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Yona mwana wa Amitai: Neno: Maandiko Matakatifu Neno la bwana lilimjia Yona mwana wa Amitai: BIBLIA KISWAHILI Basi neno la BWANA lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, |
Yeye akaurudisha mpaka wa Israeli toka kuingia kwa Hamathi hata bahari ya Araba, sawasawa na neno la BWANA, Mungu wa Israeli, alilolinena kwa mkono wa mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii, aliyekuwa wa Gath-heferi.
Simba amekwisha kunguruma, ni nani asiyeogopa? Bwana MUNGU amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri?
Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake.
Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.