Yohana 9:32 - Swahili Revised Union Version Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya mtu, ambaye alizaliwa kipofu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu. Biblia Habari Njema - BHND Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu. Neno: Bibilia Takatifu Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu. Neno: Maandiko Matakatifu Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu. BIBLIA KISWAHILI Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya mtu, ambaye alizaliwa kipofu. |
Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye.
Wengine wakasema, Maneno hayo siyo ya mtu mwenye pepo. Je! Pepo aweza kuwafumbua macho vipofu?
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapajawa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.