Yohana 6:47 - Swahili Revised Union Version Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye anao uzima wa milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uhai wa milele. Biblia Habari Njema - BHND Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uhai wa milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uhai wa milele. Neno: Bibilia Takatifu Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. Neno: Maandiko Matakatifu Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. BIBLIA KISWAHILI Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye anao uzima wa milele. |
Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma ana uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.