Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yohana 5:15 - Swahili Revised Union Version

Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Huyo mtu akaenda, akawaambia viongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ndiye aliyemponya.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Huyo mtu akaenda, akawaambia viongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ndiye aliyemponya.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Huyo mtu akaenda, akawaambia viongozi wa Wayahudi kwamba Yesu ndiye aliyemponya.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Yule mtu akaenda, akawaambia wale viongozi wa Wayahudi kuwa ni Isa aliyemponya.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Isa aliyemponya.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yohana 5:15
12 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.


Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?


Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Inawezekana kuwa huyu ndiye Kristo?


Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.


Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?


Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.


Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,


Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.


Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nilikuwa kipofu na sasa naona.


Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho!


Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.