Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
Yohana 3:7 - Swahili Revised Union Version Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usistaajabu kwamba nimekuambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. Biblia Habari Njema - BHND Usistaajabu kwamba nimekuambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usistaajabu kwamba nimekuambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo usishangae ninapokuambia, ‘Huna budi kuzaliwa mara ya pili.’ Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’ BIBLIA KISWAHILI Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. |
Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?
Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa inakuja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.
Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo.