Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hadi kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia.
Yohana 20:10 - Swahili Revised Union Version Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani. Biblia Habari Njema - BHND Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani. Neno: Bibilia Takatifu Kisha hao wanafunzi wakaondoka, wakarudi nyumbani mwao. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha hao wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao. BIBLIA KISWAHILI Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao. |
Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hadi kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia.
Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Wakati alipokuwa akilia, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi.