akisema, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi, nao watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa Mataifa,
Yohana 18:30 - Swahili Revised Union Version Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.” Biblia Habari Njema - BHND Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.” Neno: Bibilia Takatifu Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu, tusingemleta kwako.” Neno: Maandiko Matakatifu Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu tusingemleta kwako.” BIBLIA KISWAHILI Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako. |
akisema, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi, nao watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa Mataifa,
akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulubiwa, na kufufuka siku ya tatu.
Basi Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu.
Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari.
Mungu wa Abrahamu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.
Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.
Lakini pasiwe na hata mmoja wenu atakayeteseka kwa kuwa mwuaji, mwizi, mhalifu au hata mfitini.