Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
Yohana 14:14 - Swahili Revised Union Version Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni. Biblia Habari Njema - BHND Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni. Neno: Bibilia Takatifu Mkiniomba lolote kwa Jina langu, nitalifanya. Neno: Maandiko Matakatifu Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya. BIBLIA KISWAHILI Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya. |
Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu.
Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu;