Alipotoka akiwa hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu.
Yohana 13:24 - Swahili Revised Union Version Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Simoni Petro akamwashiria na kusema: “Mwulize anasema juu ya nani.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, Simoni Petro akamwashiria na kusema: “Mwulize anasema juu ya nani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Simoni Petro akamwashiria na kusema: “Mwulize anasema juu ya nani.” Neno: Bibilia Takatifu Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.” Neno: Maandiko Matakatifu Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.” BIBLIA KISWAHILI Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye? |
Alipotoka akiwa hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu.
wakawapungia mikono washiriki wenzao waliokuwa katika mashua nyingine, waje kuwasaidia; wakaja, wakazijaza mashua zote mbili, hata zikakaribia kuzama.
Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.
Paulo akasimama, akawapungia mkono, akasema, Enyi Waisraeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni.
Basi, alipompa ruhusa, Paulo akasimama madarajani, akawapungia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania.