Nilimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.
Yohana 12:8 - Swahili Revised Union Version Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamko nami sikuzote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote.” Biblia Habari Njema - BHND Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote.” Neno: Bibilia Takatifu Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.” Neno: Maandiko Matakatifu Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.” BIBLIA KISWAHILI Kwa maana maskini mnao siku zote pamoja nanyi; bali mimi hamko nami siku zote. |
Nilimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.
maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamko nami sikuzote.
Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.
Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamuwezi kuja.
Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.