Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
Yohana 12:10 - Swahili Revised Union Version Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro, Biblia Habari Njema - BHND Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro, Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakapanga njama ya kumuua Lazaro pia, Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, BIBLIA KISWAHILI Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye; |
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.
Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi.
Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishika hata mtu akifufuka katika wafu.
Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua alipo, alete habari, ili wapate kumkamata.
Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu.