Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
Yohana 11:10 - Swahili Revised Union Version Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maana mwanga haumo ndani yake.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maana mwanga haumo ndani yake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mtu akitembea usiku atajikwaa kwa maana mwanga haumo ndani yake.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini wale wanaotembea usiku hujikwaa kwa sababu hawana nuru ndani yao.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wale watembeao usiku hujikwaa kwa sababu hakuna nuru ndani yao.” BIBLIA KISWAHILI Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. |
Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.
Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.
Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.