Yohana 10:40 - Swahili Revised Union Version Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akaenda tena ngambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko. Biblia Habari Njema - BHND Yesu akaenda tena ngambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akaenda tena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko. Neno: Bibilia Takatifu Isa akaenda tena ng’ambo ya Yordani hadi mahali Yahya alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. Neno: Maandiko Matakatifu Akaenda tena ng’ambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yahya alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. BIBLIA KISWAHILI Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko. |
Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.
Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua.