Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
Yohana 10:13 - Swahili Revised Union Version Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. Biblia Habari Njema - BHND Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. Neno: Bibilia Takatifu Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo. BIBLIA KISWAHILI Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. |
Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwizi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu.
Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;