Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Yohana 1:5 - Swahili Revised Union Version Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. Biblia Habari Njema - BHND Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. Neno: Bibilia Takatifu Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda. Neno: Maandiko Matakatifu Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda. BIBLIA KISWAHILI Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. |
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.