Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Yoeli 2:29 - Swahili Revised Union Version tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata juu ya watumishi wa kiume na wa kike, nitaimimina roho yangu wakati huo. Biblia Habari Njema - BHND Hata juu ya watumishi wa kiume na wa kike, nitaimimina roho yangu wakati huo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata juu ya watumishi wa kiume na wa kike, nitaimimina roho yangu wakati huo. Neno: Bibilia Takatifu Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho wangu Mtakatifu. Neno: Maandiko Matakatifu Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho wangu. BIBLIA KISWAHILI tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. |
Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema BWANA.
Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimdunga; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wagiriki; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.