Yoeli 1:6 - Swahili Revised Union Version Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye nguvu, tena halina hesabu; Meno yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya simba mkubwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jeshi la nzige limeivamia nchi yetu; lina nguvu na ni kubwa ajabu; meno yake ni kama ya simba, na magego yake ni kama ya simba jike. Biblia Habari Njema - BHND Jeshi la nzige limeivamia nchi yetu; lina nguvu na ni kubwa ajabu; meno yake ni kama ya simba, na magego yake ni kama ya simba jike. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jeshi la nzige limeivamia nchi yetu; lina nguvu na ni kubwa ajabu; meno yake ni kama ya simba, na magego yake ni kama ya simba jike. Neno: Bibilia Takatifu Taifa limevamia nchi yangu, lenye nguvu tena lisilo na idadi; lina meno ya simba, magego ya simba jike. Neno: Maandiko Matakatifu Taifa limevamia nchi yangu, lenye nguvu tena lisilo na idadi; lina meno ya simba, magego ya simba jike. BIBLIA KISWAHILI Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye nguvu, tena halina hesabu; Meno yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya simba mkubwa. |
Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe;
naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hadi shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.
Hawatakaa katika nchi ya BWANA; lakini Efraimu atarudi Misri, nao watakula chakula najisi katika Ashuru.
Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.