Yobu 10:3 - Swahili Revised Union Version Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, ni sawa kwako kunionea, kuidharau kazi ya mikono yako na kuipendelea mipango ya waovu? Biblia Habari Njema - BHND Je, ni sawa kwako kunionea, kuidharau kazi ya mikono yako na kuipendelea mipango ya waovu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, ni sawa kwako kunionea, kuidharau kazi ya mikono yako na kuipendelea mipango ya waovu? Neno: Bibilia Takatifu Je, inakupendeza wewe kunidhulumu, kuikataa kazi ya mikono yako, huku ukiunga mkono mipango ya waovu? Neno: Maandiko Matakatifu Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu? BIBLIA KISWAHILI Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuiunga mkono mipango ya waovu? |
Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema; Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?
Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?
Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
BWANA atanitimizia malengo yake kwangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiiache kazi ya mikono yako.
Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako.
Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.