Yakobo 2:4 - Swahili Revised Union Version je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo maovu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya? Biblia Habari Njema - BHND je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya? Neno: Bibilia Takatifu je, hamjabagua kati yenu wenyewe na kuwa mahakimu wenye mawazo maovu? Neno: Maandiko Matakatifu je, hamjawabagua na kuwa mahakimu mioyoni mwenu mkihukumu kwa mawazo yenu maovu? BIBLIA KISWAHILI je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo maovu? |
Sembuse yeye huwajali nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,
Kwa sababu hiyo mimi nami nimewafanya ninyi kuwa kitu cha kudharauliwa, na unyonge, mbele ya watu wote, kama vile ninyi msivyozishika njia zangu, bali mmewapendelea watu katika sheria.
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.