nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisatikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.
Walawi 9:21 - Swahili Revised Union Version na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA; kama Musa alivyoagiza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini vile vidari na ule mguu wa nyuma wa kulia, Aroni alifanya navyo ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu, kama Mose alivyoamuru. Biblia Habari Njema - BHND Lakini vile vidari na ule mguu wa nyuma wa kulia, Aroni alifanya navyo ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu, kama Mose alivyoamuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini vile vidari na ule mguu wa nyuma wa kulia, Aroni alifanya navyo ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu, kama Mose alivyoamuru. Neno: Bibilia Takatifu Haruni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za Mwenyezi Mungu ili viwe sadaka ya kuinuliwa, kama Musa alivyoagiza. Neno: Maandiko Matakatifu Haruni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za bwana ili viwe sadaka ya kuinuliwa, kama Musa alivyoagiza. BIBLIA KISWAHILI na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kama Musa alivyoagiza. |
nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisatikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.
Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa matumizi mengine; lakini msiyale kamwe.
Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,
Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.