Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa sababu umemwachilia atoke mkononi mwako mtu niliyemweka ili aangamizwe kabisa, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, na watu wako mahali pa watu wake.
Walawi 20:4 - Swahili Revised Union Version Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yoyote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama wananchi wa mahali hapo hawatamwadhibu mtu huyo kwa kumuua, Biblia Habari Njema - BHND Kama wananchi wa mahali hapo hawatamwadhibu mtu huyo kwa kumuua, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama wananchi wa mahali hapo hawatamwadhibu mtu huyo kwa kumuua, Neno: Bibilia Takatifu Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho yao wakati mtu huyo anapomtoa kafara mmoja wa watoto wake kwa Moleki, nao wakaacha kumuua, Neno: Maandiko Matakatifu Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho wakati mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, nao wakaacha kumuua, BIBLIA KISWAHILI Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yoyote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue; |
Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa sababu umemwachilia atoke mkononi mwako mtu niliyemweka ili aangamizwe kabisa, roho yako itakuwa mahali pa roho yake, na watu wako mahali pa watu wake.
Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, na nitamtenga na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.
ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamtenga na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao.
Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.
usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;
Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie kikwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.