Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.
Walawi 18:12 - Swahili Revised Union Version Usifunue utupu wa dada ya baba yako; maana, yeye ni jamaa wa karibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kamwe usilale na shangazi yako; kwani huyo ni dada wa baba yako. Biblia Habari Njema - BHND Kamwe usilale na shangazi yako; kwani huyo ni dada wa baba yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kamwe usilale na shangazi yako; kwani huyo ni dada wa baba yako. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako. BIBLIA KISWAHILI Usifunue utupu wa dada ya baba yako; maana, yeye ni jamaa wa karibu. |
Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.
Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni dada yako, usifunue utupu wake.
Usifunue utupu wa dada ya mama yako, wala dada ya baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watalipizwa kwa uovu wao.