Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
Walawi 17:9 - Swahili Revised Union Version wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa BWANA basi mtu huyo atatengwa na watu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema lakini haileti mbele ya mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atatengwa na watu wake. Biblia Habari Njema - BHND lakini haileti mbele ya mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atatengwa na watu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza lakini haileti mbele ya mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atatengwa na watu wake. Neno: Bibilia Takatifu bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. Neno: Maandiko Matakatifu bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwa bwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. BIBLIA KISWAHILI wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa BWANA basi mtu huyo atatengwa na watu wake. |
Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.
Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.
wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, kama matoleo kwa BWANA mbele ya hema ya BWANA; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na atatupiliwa mbali na watu wake;
Nawe utawaambia, Mtu yeyote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu,