Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Walawi 13:25 - Swahili Revised Union Version

ndipo kuhani atapaangalia; ikiwa nywele iliyo katika kile kipaku imegeuka kuwa nyeupe, na kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe; ni ukoma, umetokea katika mahali palipoungua; na kuhani atasema kuwa ni najisi; hili ni pigo la ukoma.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

kuhani atapaangalia. Kama akiona kuwa nywele zimegeuka kuwa nyeupe na pana shimo, basi, huo ni ukoma. Ukoma huo umejitokeza kwa njia ya mahali hapo palipoungua. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani anao ugonjwa wa ukoma.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

kuhani atapaangalia. Kama akiona kuwa nywele zimegeuka kuwa nyeupe na pana shimo, basi, huo ni ukoma. Ukoma huo umejitokeza kwa njia ya mahali hapo palipoungua. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani anao ugonjwa wa ukoma.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

kuhani atapaangalia. Kama akiona kuwa nywele zimegeuka kuwa nyeupe na pana shimo, basi, huo ni ukoma. Ukoma huo umejitokeza kwa njia ya mahali hapo palipoungua. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; kwani anao ugonjwa wa ukoma.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

kuhani ataichunguza ile alama, na kama nywele zilizo juu yake zimegeuka kuwa nyeupe, na panaonekana kuingia ndani ya ngozi, basi huo ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza ambao umetokea katika jeraha la moto. Kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

kuhani ataichunguza ile alama, na kama nywele zilizoko juu yake zimegeuka kuwa nyeupe, napo pametokea shimo, basi huo ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza ambao umetokea juu ya jeraha la moto. Kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

ndipo kuhani atapaangalia; ikiwa nywele zilizopo katika kile kipaku zimegeuka kuwa nyeupe, na kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe; ni ukoma, umetokea katika mahali palipoungua; na kuhani atasema kuwa ni najisi; hili ni pigo la ukoma.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Walawi 13:25
7 Marejeleo ya Msalaba  

Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.


BWANA akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! Mkono wake ulikuwa una ukoma, umekuwa mweupe kama theluji.


Au mwili wa mtu ukiwa una mahali palipoungua katika ngozi yake, kisha pakawa kidonda, kikawa kipaku chekundu kidogo, au cheupe;


Lakini kuhani akipaangalia, nywele nyeupe hamna katika hicho kipaku king'aacho, nacho hakikuingia ndani kuliko ngozi, lakini chafifia; ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba;


Lakini ikiwa kipaku king'aacho katika ngozi ya mwili wake ni cheupe, na kuonekana si shimo la kuingia ndani kuliko ngozi wala nywele hazikugeuka kuwa nyeupe, ndipo kuhani atamweka mahali muda wa siku saba huyo aliye na hilo pigo;


Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na na kumwona akiwa mwenye ukoma.