Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Walawi 1:2 - Swahili Revised Union Version

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa kufugwa, katika ng'ombe, kondoo na mbuzi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Waambie Waisraeli kwamba kama mtu anapenda kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya mnyama, mnyama huyo atamchagua kutoka kundi lake la ng'ombe, kondoo au mbuzi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Waambie Waisraeli kwamba kama mtu anapenda kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya mnyama, mnyama huyo atamchagua kutoka kundi lake la ng'ombe, kondoo au mbuzi.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Waambie Waisraeli kwamba kama mtu anapenda kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya mnyama, mnyama huyo atamchagua kutoka kundi lake la ng'ombe, kondoo au mbuzi.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Sema na Waisraeli, uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu anayeleta sadaka kwa Mwenyezi Mungu, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ng’ombe, au la kondoo na mbuzi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwa bwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ng’ombe au la kondoo na mbuzi.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa kufugwa, katika ng'ombe, kondoo na mbuzi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Walawi 1:2
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.


bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.


Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, na mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;


na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za BWANA, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea BWANA sadaka kwa hiari yake.


Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.


nanyi mwataka kumsogezea BWANA sadaka kwa moto, kwamba ni sadaka ya kuteketezwa, au dhabihu ya kuchinjwa, ili kuondoa nadhiri, au iwe sadaka ya hiari, au katika sikukuu zenu zilizoamriwa, ili kumfanyia BWANA harufu ipendezayo, katika ng'ombe, au katika kondoo;


ndipo huyo mume atamchukua mkewe, aende naye kwa kuhani, naye ataleta sadaka yake kwa ajili yake, yaani, sehemu ya kumi ya efa; asitie mafuta juu yake, wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho ya kukumbukia uovu.


ng'ombe dume mchanga, mmoja na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa;


Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu chochote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;


Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.


Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa ni unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;


mkaende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.