Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.
Wafilipi 1:4 - Swahili Revised Union Version sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na kila ninapowaombeeni nyote, nasali kwa furaha, Biblia Habari Njema - BHND na kila ninapowaombeeni nyote, nasali kwa furaha, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na kila ninapowaombeeni nyote, nasali kwa furaha, Neno: Bibilia Takatifu Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, Neno: Maandiko Matakatifu Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, BIBLIA KISWAHILI siku zote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha, |
Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.
Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.
Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma,
ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkiwaza mamoja.
Maana wengi huenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji langu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.
Maana nilikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu.
Nilifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.