Maana wewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na hadharani.
Waefeso 5:12 - Swahili Revised Union Version kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. Biblia Habari Njema - BHND Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. BIBLIA KISWAHILI kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena. |
Maana wewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na hadharani.
Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.
katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na Injili yangu, kwa Kristo Yesu.
Lakini chochote kinachoangazwa na nuru hudhihirishwa, maana chochote kile kilichoadhihirika ni nuru.
Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu;
Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, kulingana na matendo yao.