Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya BWANA pamoja nanyi katika maneno haya yote.
Waebrania 9:20 - Swahili Revised Union Version akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose alisema: “Hii ni damu inayothibitisha agano mliloamriwa na Mungu mlitii.” Biblia Habari Njema - BHND Mose alisema: “Hii ni damu inayothibitisha agano mliloamriwa na Mungu mlitii.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose alisema: “Hii ni damu inayothibitisha agano mliloamriwa na Mungu mlitii.” Neno: Bibilia Takatifu Alisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” Neno: Maandiko Matakatifu Alisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mwenyezi Mungu amewaamuru kulitii.” BIBLIA KISWAHILI akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. |
Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya BWANA pamoja nanyi katika maneno haya yote.
Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji.
kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
ili uingie katika agano la BWANA, Mungu wako, na kiapo chake, afanyacho nawe BWANA, Mungu wako, hivi leo;
Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,
Nao wakamwendea Yoshua hadi kambini huko Gilgali, nao wakamwambia yeye na watu wa Israeli, Sisi tumetoka nchi ya mbali sana; basi kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi.