Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Waebrania 13:13 - Swahili Revised Union Version Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutuma yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. Biblia Habari Njema - BHND Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba. BIBLIA KISWAHILI Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutuma yake. |
Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.
Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.
Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo.
Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na matusi, na matatizo, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili upinzani mkuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.
mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.