Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.
Waebrania 11:18 - Swahili Revised Union Version naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ingawa Mungu alikuwa amemwambia: “Wazawa wako watatokana na Isaka.” Biblia Habari Njema - BHND ingawa Mungu alikuwa amemwambia: “Wazawa wako watatokana na Isaka.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ingawa Mungu alikuwa amemwambia: “Wazawa wako watatokana na Isaka.” Neno: Bibilia Takatifu hata ingawa Mungu alikuwa amemwambia Ibrahimu, “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwa Isaka.” Neno: Maandiko Matakatifu Ingawa Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Ibrahimu, “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwa Isaka,” BIBLIA KISWAHILI naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, |
Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.
Mungu akamwambia Abrahamu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazawa wa Abrahamu, bali, Katika Isaka wazawa wako wataitwa;
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,