Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu?
Waebrania 10:3 - Swahili Revised Union Version Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini tambiko hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao. Biblia Habari Njema - BHND Lakini tambiko hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini tambiko hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao. Neno: Bibilia Takatifu Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, BIBLIA KISWAHILI Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. |
Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu?
Naye Haruni atafanya upatanisho juu ya pembe zake mara moja kila mwaka; kwa damu ya ile sadaka ya dhambi ya kufanya upatanisho, mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote; ni takatifu sana kwa BWANA.
Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye akafanya vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa.
kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi walizozitenda hao watu bila kujua.