Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Waebrania 1:13 - Swahili Revised Union Version Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono wa kulia Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.” Biblia Habari Njema - BHND Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.” Neno: Bibilia Takatifu Je, ni kwa malaika yupi Mungu aliwahi kusema, “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako”? Neno: Maandiko Matakatifu Je, ni kwa malaika yupi ambaye Mwenyezi Mungu amepata kumwambia wakati wowote, “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako”? BIBLIA KISWAHILI Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono wa kulia Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? |
Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi katika mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?
Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Maana, Daudi mwenyewe asema katika kitabu cha Zaburi, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kulia,
Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kulia wa Mungu.
Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;
Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemadari wa watu wa vita waliokwenda naye, Haya, jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao.
Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.