Waebrania 1:12 - Swahili Revised Union Version Na kama mavazi utazikunjakunja, na kama mavazi zitabadilishwa; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.” Biblia Habari Njema - BHND Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.” Neno: Bibilia Takatifu Utazikunjakunja kama joho, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe hubadiliki, nayo miaka yako haikomi kamwe.” Neno: Maandiko Matakatifu Utazikung’utakung’uta kama joho, nazo zitachakaa kama vazi. Lakini wewe hubadiliki, nayo miaka yako haikomi kamwe.” BIBLIA KISWAHILI Na kama mavazi utazikunjakunja, na kama mavazi zitabadilishwa; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma. |
Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.
Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.
Makao yangu yameondolewa kabisa, yamechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.