Ufunuo 20:1 - Swahili Revised Union Version Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Neno: Bibilia Takatifu Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa ameshika ufunguo wa lile Shimo na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa ameshika ufunguo wa lile Shimo na mnyororo mkubwa mkononi mwake. BIBLIA KISWAHILI Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. |
Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.
Baada ya hayo niliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia mhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe kwa muda mfupi.