Ruthu 1:10 - Swahili Revised Union Version Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutarudi pamoja nawe kwa watu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na kumwambia, “La hasha! Tutakwenda pamoja nawe kwa watu wako.” Biblia Habari Njema - BHND na kumwambia, “La hasha! Tutakwenda pamoja nawe kwa watu wako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na kumwambia, “La hasha! Tutakwenda pamoja nawe kwa watu wako.” Neno: Bibilia Takatifu wakamwambia, “Tutarudi pamoja na wewe kwa watu wako.” Neno: Maandiko Matakatifu wakamwambia, “Tutarudi pamoja na wewe nyumbani kwa watu wako.” BIBLIA KISWAHILI Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutarudi pamoja nawe kwa watu wako. |
BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yuko pamoja nanyi.
Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, rudini; kwa nini mfuatane nami? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu?
Basi akatoka pale alipokuwa akiishi, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda.
BWANA na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia.