BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.
Obadia 1:2 - Swahili Revised Union Version Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu aliambia taifa la Edomu: “Nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa, utadharauliwa kabisa na wote. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu aliambia taifa la Edomu: “Nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa, utadharauliwa kabisa na wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu aliambia taifa la Edomu: “Nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa, utadharauliwa kabisa na wote. Neno: Bibilia Takatifu “Tazama, nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa, utadharauliwa kabisa. Neno: Maandiko Matakatifu “Angalieni, nitawafanya wadogo miongoni mwa mataifa, mtadharauliwa kabisa. BIBLIA KISWAHILI Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana. |
BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.
Utakuwa duni kuliko falme zote; wala hautajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza, ili wasitawale tena juu ya mataifa.
Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi BWANA, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu.
Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.