Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Nehemia 9:7 - Swahili Revised Union Version Wewe ndiwe BWANA, Mungu, uliyemchagua Abramu, na kumtoa katika Uri wa Wakaldayo, na kumpa jina la Abrahamu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu uliyemchagua Abramu, ukamtoa toka Uri ya Wakaldayo na kumpa jina Abrahamu. Biblia Habari Njema - BHND Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu uliyemchagua Abramu, ukamtoa toka Uri ya Wakaldayo na kumpa jina Abrahamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu uliyemchagua Abramu, ukamtoa toka Uri ya Wakaldayo na kumpa jina Abrahamu. Neno: Bibilia Takatifu “Wewe ni Bwana Mwenyezi Mungu uliyemchagua Abramu na kumtoa kutoka Uru ya Wakaldayo, nawe ukamwita Ibrahimu. Neno: Maandiko Matakatifu “Wewe ni bwana Mwenyezi Mungu uliyemchagua Abramu na kumtoa kutoka Uru ya Wakaldayo, nawe ukamwita Ibrahimu. BIBLIA KISWAHILI Wewe ndiwe BWANA, Mungu, uliyemchagua Abramu, na kumtoa katika Uri wa Wakaldayo, na kumpa jina la Abrahamu; |
Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uimiliki.
wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Abrahamu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nilimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
Tena, BWANA aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo.